Katibu
Mkuu wa zamani wa Simba, Kassim Dewji amewataka mashabiki wa Msimbazi
kutotegemea mambo makubwa sana katika mechi yao ya Oktoba 18 dhidi ya Yanga.
Dewji
ambaye yuko Johannesburg, Afrika Kusini ambako kikosi cha Simba kimeweka kambi,
amesema bado kuna mambo mengi yanapaswa kubadilishwa.
“Kikosi
hiki kina mambo mengi ambayo unayaona kadiri siku zinavyokwenda, uongozi
unafanya juhudi, benchi la ufundi linajituma.
“Unajua,
kunamabadiliko yanafanyika na kawaida kwenye mabadiliko kunahitaji muda,
haiwezi kuwa mara moja tu kila kitu kinabadilika.
“Mechi
inayokuja dhidi ya Yanga, mashabiki wasitarajie makubwa sana kutokana na hali
hii,” alisema Dewji.
“Lakini
haina maana timu itaingia uwanjani kwenda kufungwa, tutapambana kwa kuwa ndiyo
utamaduni wa Simba, kupambana na kuwapa heshima mashabiki na wanachama.
“Ndiyo
maana nasisitiza kutotegemea makubwa sana, watu waamini timu bado
inabadilishwa, inapita kipindi kigumu cha mpito kutoka katika kipindi ambacho
Simba iliporomoka, hivyo tuwe wavumilivu kidogo, tuuamini uongozi, tuwaamini
watu wa benchi la ufundi.”
Simba
inatarajia kucheza mechi yake ya kirafiki kesho dhidi ya Jomo Cosmos.







0 COMMENTS:
Post a Comment