October 14, 2014


Simba itacheza mechi yake ya mwisho ya kirafiki kesho dhidi ya Jomo Cosmos.

Mechi hiyo itapigwa jijini Johannesburg na baada ya hapo Simba itaanza safari ya kutejea Dar es Salaam.
Simba iko kwenye maandalizi ya mechi dhidi ya watani wake Yanga, Oktoba 18.

Mmoja wa viongozi wa Kundi la Friends of Simba, Kassim Dewji amesema maandalizi yanaendelea vizuri.
“Tuko hapa, timu imefanya mazoezi leo na na kesho ndiyo mechi ya mwisho.

“Hakika vijana wanaendelea vizuri ndiyo maana tumefungas afari tupo hapa kuungana nao,” alisema.

Tayari Simba imecheza mechi mbili za kirafiki, dhidi ya Orlando Pirates ambayo ilitoka sare ya ya bila kufungana kabla ya kupata kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa Wits.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic