MANJI |
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amelishauri
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuiangalia adhabu ya kumfungia miaka saba
mwanasheria Dk Damas Daniel Ndumbaro asijihusishe na masuala ya soka.
Manji ameiambia TFF wakati ilipokutana na
viongozi wa juu wa klabu za Ligi Kuu Bara, juzi kabla ya Yanga na Simba
hazijavaana.
Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao
hicho zimeeleza, Manji alimshauri Malinzi kuiangalia adhabu hiyo ya Dk Ndumbaro
kwa kuwa kujenga familia ya soka si kufungiana.
DK NDUMBARO |
“Manji amewaambia TFF kwamba hakuna sababu
ya kufungiana, kama kuna hali ya kutoelewana, iko haja ya kujadiliana na
kufikia mwafaka,” kilieleza chanzo.
“Manji alisema hayo wakati akichangia mambo
kadhaa, hata hivyo mkutano haukuwa mrefu sana, watu wakakimbilia mpirani,”
kilisisitiza chanzo.
Dk Ndumbaro ambaye ni daktari wa sheria yuko
nchini Marekani kwa mwaliko wa moja ya vyuo vikuu nchini humo, alifungiwa baada
ya kuzitetea klabu zisikatwe asilimia tano kutoka kwenye fedha za wadhamini.
Wakati anafungiwa, Dk Ndumbaro ambaye
hakusikilizwa, alikuwa tayari ameondoka nchini kwenda Marekani.
Huyo Ndumbaro hana tofauti na Dr.Majimarefu wa Simba tuu!
ReplyDelete