October 20, 2014


Mdau Abdulfatah Saleh, ameamua kuingia gym na kujifua vilivyo.

Abdulfatah ambaye ni mmoja wa wadau maarufu wa mchezo wa soka nchini, amesema uamuzi wake wa kuingia gym si kwamba ana pambano la ngumi au anataka kujiunga na kikosi cha Simba, Yanga au Azam FC kutokana na kuwa na umbo zuri la upachikaji mabao.
Badala yake ameamua kufanya hivyo kujiweka fiti pia kujitahidi kuepuka magonjwa.
"Mazoezi ni kitu kizuri, hata kama tunabanwa na kazi, vizuri kujiweka vizuri.
"Mazoezi yanaumiza, hakika yanataka uvumilivu lakini ni vizuri kwa kuwa siku hizi magonjwa pia ni mengi," alisema Abdulfatah ambaye ni mmiliki wa hoteli maarufu ya Sapphire Court ya jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic