October 7, 2014



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema kikosi chao hakina hofu hata kidogo na watani wa jadi Yanga kwa kuwa wanakwenda kimungumungu.


Hans Poppe amesema Simba haina sababu ya kuihofia Yanga ambayo itapambana nayo Oktoba 18 kwa kuwa inakwenda kwa kubahatisha.
"Inakwenda kimungumungu, sasa utaona ni kawaida tu na hakuna kinachotisha.
"Utaona wanasema maneno kuwa ni wakali, sasa mechi ipi wamefanya vizuri na kushinda. Hakuna cha kuwahofia Yanga.
"Halafu lazima ujue mechi za watani wa jadi hazijali nani yuko fiti na nani yuko vipi," alisema Hans Poppe na kuongeza.
"Angalia kwenye mechi ya Mtani Jembe, hatukuwa kwenye kiwango kizuri lakini tukawachapa tatu."
Simba imeanza kwa sare tatu mfululizo, wakati Yanga ilianza kwa kipigo na sasa imeshinda mechi mbili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic