Hatimaye kesi ya mauaji
iliyokuwa inamkabiri mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius imefikia tamati kwa
yeye kuhukumiwa miaka mitano jela.
Pistorius aliyekuwa
anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp amehukumiwa kwenda jela miaka
mitano kwa kesi ya mauaji bila ya kukusudia.
Awali mwanariadha huyo
aliondolewa mashitaka ya kuua kwa kukusudia.
Akiwa mahakani leo mjini
Pretoria, aliangua kilio baada ya hukumu hiyo.
Hata hivyo, mama mzazi wa
marehemu, alipinga na kusema adhabu hiyo ni ndogo.
Pia taasisi za kutetea haki
za binadamu zimekuwa zikipinga kwa kasi kubwa kuhusiana na hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment