Idriss Ally, Mwanza
Kocha
Mkuu wa Mwadui ya Shinyanga, Jamhuri Kihwelo amesema kipigo cha bao 1-0
walichokipata kutoka kwa Toto African si mwisho wa safari.
Katika
mechi hiyo ya Ligi Daraja la Kwanza iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
mjini hapa, bao pekee la wenyeji lilifungwa na Andusi Issa katika dakika ya 78.
Andus
aliwatoka mabeki wa Mwadui kabla ya kugeuka na kupiga mkwaju mkali kutoka mita
22, ukajaa wavuni.
“Utaona
mechi hii ilikuwa yetu, tumepoteza nafasi nyingi na tulikuwa na nafasi ya
kushinda.
“Lakini
huu si mwisho wa safari, bado tuna njia ya kupita na kufanya vizuri zaidi,”
alisema Julio.
Mechi nyingine ya Ligi Daraja la Kwanza iliyochezwa leo jijini Dar es Salaam, Friends Rangers ya Magomeni Kagera iliitungua Lipuli kwa mabao 2-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment