Kocha
Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amewaambia wachezaji wake kuwa kuna kitu amekiona
baada ya sare dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Simba
imetoka sare ya bila kufungana dhidi ya Orlando Pirates katika mechi ya
kirafiki iliyochezwa leo jijini Johannesburg.
Simba iliwakosa wachezaji wake walio kwenye kikosi cha Taifa Stars pia Emmanuel Okwi ambaye ameitumikia Uganda, leo.
Phiri
raia wa Zambia, amewaambia wachezaji wake kuwa moja ya kitu alichokiona ni hali
ya kujiamini kurejea.
“Kocha
amefurahishwa na tulivyocheza, ingawa tulicheza na timu kubwa, lakini
tulionyesha kujiamini.
“Orlando
walichanganya na wachezaji kadhaawa timu ya vijana kwa kuwa wachezaji wao
wengine walikuwa wamekwenda kuitumikia timu yao ya taifa kwenye michuano ya
kuwania kuchea Kombe la Mtaifa Afrika,” kilieleza chanzo.
“Lakini
mechi ilikuwa ngumu sana, jamaa wako fiti lakini tuliwadhibiti vizuri kabisa.
“Hata
baada ya mchezo nao walifurahia na kusema ilikuwa ni mechi nzuri na
itakayowasaidia.”
Phiri
amewasisitiza wachezaji wake kuendelea kujiongeza kutoka walipo na kwenda mbele
kwa mafanikio zaidi.
Simba
imeamua kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini kutokana na mambo mawili,
kuanza kwa sare tatu mfululizo lakini kujiandaa dhidi ya Yanga Oktoba 18.
0 COMMENTS:
Post a Comment