Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema
ushindi wa mabao mengi kuanzia matano ndiyo kitu anachotaka.
Mwadui ambayo ilikuwa imekwenda sare mfululizo kwenye
mechi zake za Ligi Daraja la Kwanza iliibuka na kuichapa Polisi Mara kwa mabao
5-1.
Mwadui ndiyo ilikuwa inacheza nyumbani kwenye Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga kwa mara ya kwanza msimu huu.
Julio amesema angefurahi kuona kikosi chake kinashinda kwa
idadi hiyo ya mabao.
“Mabao matano ikiwezekana zaidi yana faida kubwa. Sema kwenye
soka hauwezi kwenda hivyo moja kwa moja.
“Kikubwa ni kwamba tunahitaji ushindi kwa ajili ya
kujiwekea mazingira mazuri ya baadaye,” alisema Julio.
Beki huyo wa zamani wa Simba, aliwapongeza wachezaji wake kwa
kuonyesha soka safi na kufunga idadi nzuri ya mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment