October 11, 2014


Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Benin.
Lakini akasisitiza, haitakuwa mechi laini kama ambavyo wengi wanafikiri.

"Tumejiandaa vizuri, tunataka kucheza mpira mzuri na kushinda, hayo ndiyo malengo.
"Lakini Benin si timu laini, hivyo tayari wachezaji wanajua wanacheza na timu ngumu lakini inafungika," alisema Nooij raia wa Uholanzi.
Stars imekuwa kambini kwa wiki moja sasa ikijiandaa na mechi hiyo.
Kikosi hicho kitamkosa Mbwana Samatta ambaye aliumia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiitumikia TP Mazembe ya DR Congo ambayo ilitolewa kwenye hatua ya nusu fainali.
Nyota wa nje watakaokuwa kwenye kikosi hicho ni pamoja na Thomas Ulimwengu (TP-DR Congo), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya-Qatar) na Juma Luizio (Zesco-Zambia).

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic