Mambo yameendelea kuwa magumu baada ya
Liverpool kuchapwa nyumbani kwa mabao 3-0 katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Real Madrid ndiyo walioingusha Liverpool
ikiwa nyumbani na Cristiano Ronaldo akapiga bao la kwanza kabla Mfaransa, Karim
Benzema kutupia mbili.
Juhudi za Liverpool kutaka kusawazisha
katika kipindi cha pili hazikuzaa matunda. Mshambuliaji wa Liverpool, Mario Balotelli alionekana kufanya juhudi, lakini hakufurukuta.
0 COMMENTS:
Post a Comment