October 2, 2014


Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema ni lazima klabu zikatwe fedha zao za udhamini.

TFF iliagiza klabu zote 14 za Ligi Kuu Bara, zikatwe fedha zao za udhamini kutoka Vodacom na Azam TV.
Agizo hilo, liliamsha hisia za klabu ambazo zilisisitiza kwamba haziwezi kukubali hali.
Hali iliyosababisha Mbeya City na Mtibwa Sugar, kutishia kwenda mahakamani.
Akizungumza leo, Malinzi alisema lazima fedha hizo zikatwe kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya soka.
"Hilo suala la kukatwa fedha limeishapita, ni agizo na lazima litekelezwe," alisema Malinzi.
Klabu pia zimekuwa zikikatwa fedha zao za mapato na fedha kwenda kwenye mfuko wa maendeleo.

2 COMMENTS:

  1. Safi sana Jamal malinzi kwa kujali maendeleo ya soka TZ,kila siku tunalalamika kuhusu kuendeleza vipaji vya vijana kulinusuru taifa dhidi ya aibu ya kufungwa kila siku,sasa Jamal amejitokeza kupambana na hilo wajingajinga wanalalamika!mitanzania jamani sijuhi ipoje!?

    ReplyDelete
  2. si haki, TFF ingetafuta wadhamini wake na ikumbukwe pia kwamba udhamini huambatana na masharti na hesabu, sasa say mdhamini amedhamini usafiri wa kwenda kituo cha mechi kwa ndege badala ya usafiri wa basi wa vodacom halafu unakata asilimia tano unamaanisha nini

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic