October 20, 2014

MASAU BWIRE.
Baada ya kufanikiwa kutoka mkiani mwa Ligi Kuu Bara kwa ushindi mmoja tu, Ruvu Shooting wameanza kutamba, wakisema ndiyo kwanza wameanza ligi.


Ruvu ilifanikiwa kuiadhibu Ndanda kwa mabao 3-1 juzi ugenini kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, lakini kabla ya hapo ilikuwa imetoa sare michezo miwili na kupoteza mmoja.

Ruvu ambayo ilipoteza mchezo wake wa kwanza kwa kufungwa 2-0 na Prisons, kabla ya kupokea kipigo kingine cha mabao 2-0 kutoka kwa Azam FC, kisha ikatoka suluhu na Mbeya City, imepata ushindi wake wa kwanza msimu huu juzi.


Ofisa Habari wa Ruvu Shooting mwenye maneno mengi, Masau Bwire, alisema kutokana na kushindwa kufanya vizuri katika michezo ya awali, sasa ndiyo wameanza rasmi ligi hiyo kwa kuifunga Ndanda.
  
“Tumefanikiwa kupata ushindi wa kwanza baada ya kupoteza mechi zetu mbili za kwanza na moja kutoka sare lakini sasa ndiyo tumeanza ligi rasmi kwa sababu kabla ya kwenda Mtwara tayari tulishatoa tahadhari ya kuwa tunachukua pointi tatu ndani ya Dimba la Nangwanda Sijaona na ndicho kilichotokea, sasa wengine wakae pembeni kwani Ruvu tunakuja.






“Licha ya kuishinda Ndanda lakini walijitahidi kucheza vizuri ingawa uwezo wao ulikuwa umeishia kupata bao moja kwa sababu walikuwa wamekutana na timu ambayo inajua kucheza mpira wenye ubora mkubwa lakini mara nyingi tumekuwa tukiambiwa na watu kuwa Ruvu tunapiga kelele kama waimba taarabu, sasa niwaambie kuwa ndiyo tumenzia pale Nangwanda Sijaona,” alisema Bwire.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic