Neymar anaifukuzia rekodi ya gwiji
la soka duniani, Pele baada ya kupachika mabao manne katika mechi kati ya
Brazil dhidi ya Japan.
Kutokana na mabao yake hayo
manne, yamemuwezesha kufikisha mabao 40 katika mechi 58.
Neymar mwenye umri wa miaka 22,
anaisaka rekodi hiyo ya mabao 77.
Nyota huyo Barcelona ndiye
mwenye nafasi ya kuifikia rekodi ya Pele kwa maana ya wastani.
Kati ya wachezaji wanne
waliopiga bao nyingi kwa Brazil ni Pelé (77), Ronaldo (62), Romário (55) na Zico
(48).
Neymar anabaki kuwa pekee
anayeweza kufikia rekodi hiyo kwa kuwa pekee ndiye anayeendelea kucheza.








0 COMMENTS:
Post a Comment