Kazi ya ukocha ni ngumu jamani, tukubali. Mfano mzuri angalia Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo alivyokuwa akisumbuka kufuta jasho.
Kila baada ya dakika chache alikuwa akitoa kitambaa chake na kujifuta.
Ingawa alikuwa hakimbii, lakini jasho halikuisha usoni kwa Maximo wakati kikosi chake kikipambana dhidi ya watani wake Simba katika mechi iliyoisha kwa sare ya bila mabao.
0 COMMENTS:
Post a Comment