Bondia nyota Manny Pacquiao
ameweka rekodi ya kucheza mpira wa kikapu katika ligi ya kulipwa.
Pacquiao amecheza mpira wa
kikapu ikiwa ni mwezi kamili kabla ya kupanda jukwaani kutetea taji lake la WBO.
Bondia huyo ameichezea timu
ya KIA Sorento katika ligi ya kulipwa ya mchezo huo nchini Philippine.
Mkali huyo mwenye miaka 35
alicheza kwa dakika saba na kuandika rekodi hiyo na kuisaidia timu hiyo kuibuka
na ushindi wa pointi 80-66.
0 COMMENTS:
Post a Comment