Ushabiki mkubwa wa klabu
kubwa mbili za Hispania, Barcelona na Real Madrid, sasa umeingia kwenye sura
nyingine.
Mechi ya kesho ya El
Clasico sasa imevushwa hadi kwa wanamuziki wawili nyota wanawake.
Jennifer Lopez yeye ni Real
Madrid wakati Shakira ni Barcelona.
Jennifer na Shakira ndiyo
wamekuwa wakishindanishwa na mashabiki wao na kitendo cha kuwa timu tofauti
kimefanya mashabiki wao kuingia kwenye ushindani pia.
Kila upande umekuwa
ukitumia picha zao kuzungumzia mechi hiyo.
Katika mitandao ya kijamii,
picha zao zimejaa lukuki.
Ushindani wa mechi hiyo,
huwa mkubwa kuliko wa nyingine yoyote ya soka duniani.
0 COMMENTS:
Post a Comment