October 11, 2014

SUDAN
Sudan ndiyo timu pekee kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati iliyofanikiwa kushinda mechi yake ya kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika leo.

Sudan ikiwa imeishinda Nigeria kwa bao 1-0 lililofungwa na Bebeker katika dakika ya 42.
Lakini timu nyingine za ukanda huu, ethiopia na Uganda zote zimepoteza tena zikiwa nyumbani.
Ethiopia imepigwa bao 2-0 na Mali wakati Uganda imechapwa 1-0 na Togo.
Mechi nyingine ya jirani wa Tanzania Malawi, wakiwa nyumbani nao wamekiona cha moto kwa kuchapwa kwa mabao 2-0 na Algeria.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic