Togo
wametibua mipango ya Uganda kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika baada ya
kuwachapa kwa bao 1-0 jijini Kampala, leo.
Lakini
kama hiyo haitoshi, bao lililofungwa na Kokou Donou limeifanya The Cranes
inayoongozwa na kocha wa zamani wa Yanga, Sredejovic Milutin ‘Micho’ na
mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi kuingia kwenye kikosi cha Uganda
kilichofungwa nyumbani baada ya miaka 10 kupita.
Mara
ya mwisho, Uganda ilipoteza nyumbani kwenye michuano ya Caf mwaka 2004.
Kipigo
hicho, kimeiyumbisha Uganda ambayo ilikuwa na mwendo mzuri.
Matokeo
mengine ya leo ya michuano ya kuwania kucheza Kombe la Mataida Afrika ni haya.
Niger 0-0 Zambia
Msumbiji 2-0 Cape Verde
DR Congo 1-2 Ivory Coast
Gabon 2-0 Burkina Faso
Sierra Leone 0-0 Cameroon
Ethiopia 0-Mali 2
0 COMMENTS:
Post a Comment