MTIBWA SUGAR. |
Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru
amesema wanakwenda Mbeya kwenda kupeleka mauaji mjini Mbeya.
Kifaru amesema wataitwanga Mbeya City kwao
Mbeya kwenye mechi ya Jumapili na kuondoka na pointi tatu.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Kifaru alisema
wamejiandaa vizuri na Mbeya City wasubiri kipigo cha pili baada ya kile cha
Azam FC.
“Sisi tuko tayari, kikosi kizima kimeanza
safari ya Mbeya kwa ajili ya kupeleka mauaji hayo.
“Tutawafunga na kuendeleza kubeba pointi
tatu halafu tuondoke kwa mbwembwe,” alijigamba Kifaru.
Tayari Mbeya City imeishapoteza mchezo
nyumbani kwao Mbeya baada ya kuchapwa kwa bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment