Yanga imetoka sare ya bila kufungana katika mechi yake ya kirafiki dhidi ya CDA mjini Dodoma, leo.
Mechi hiyo imepigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na kumalizika bila bao huku mechi ikiwa na ushindani utafikiri ya ligi kuu.
Yanga iko njiani kwenda Shinyanga kupambana na Stand United katika mechi ya Ligi Kuu Bara.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema wataondoka kesho asubuhi kwenda Shinyanga tayari kabisa kwa mechi yao dhidi ya wenyeji wao Stand.
0 COMMENTS:
Post a Comment