| SEIF MAGARI AKIWA NA MWANAYE KATIKA MOJA YA MECHI ZA YANGA. |
Kocha Marcio Maximo wa
Yanga, kesho atakutana na sehemu ya uongozi wa Yanga kueleza mikakati yake.
Mwenyekiti wa kamati ya
usajili ya Yanga, Seif Ahmed ‘Magari’ amesema wanakutana na Maximo ili kujadili
maandalizi yao kwa ajili ya mechi ijayo dhidi ya Simba Oktoba 18.
Magari amesema baada ya
kukutana na Maximo na wasaidizi wake, watamsikiliza na baadaye kujadiliana.
“Mwalimu ndiye anayejua maandalizi
yanavyotakiwa kuwa, lakini tutamsikiliza na kushauriana.
“Tunajua mechi dhidi ya
Simba itakuwa ngumu, tunachotaka ni pointi tatu lakini muhimu ni kutambua ugumu
wa mechi.
“Pia tunajua mechi itakuwa
ngumu, lakini tutapambana kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Magari.
Mechi hiyo ya watani,
tayari imekuwa gumzo na mashabiki wanaisubiri kwa hamu kubwa.







0 COMMENTS:
Post a Comment