October 8, 2014


Na Saleh Ally
KASI ya wapachika mabao England inazidi kupamba moto, tumekuwa tukijaribu kuifuatilia kwa kasi kubwa.
Washambuliaji wa timu 20 za England wanachuana vikali, kila mmoja akitaka kuchukua nafasi ya ufungaji bora wa ligi hiyo.
Si kazi rahisi, ukweli uko hivi, kama ni taji sasa halina mwenyewe kwani mfungaji wa msimu uliopita, Luis Suarez aliyekwamisha mipira 31 wavuni, sasa yuko Hispania akikipiga katika kikosi cha Barcelona.
Nani atakuwa mfungaji bora? Hilo ni swali la kwanza lakini yupi ataonyesha uwezo mkubwa wa upachikaji mabao kwa kasi na uwezo wa aina yake? Nani ana kitu au vitu vya ziada katika kazi hiyo.
Ufungaji ni kipaji, mafunzo yanaweza kuongeza uwezo zaidi au utamu wakati mfungaji anausindikiza mpira wavuni kumaliza kazi yake ya hesabu ya mabao.
Kufunga mara nyingi ni sehemu tatu kuu, nyingine zinaweza kufuatia kwa ziada. Moja, mguu wa kulia, pili wa kushoto na tatu ni kichwa. Vingine, kama kifua, tumbo au vinginevyo vinaweza kutokea bila ya kutarajiwa.
Diego Costa wa Chelsea, amezidi kuonyesha kasi ya aina yake baada ya kupachika bao lake la tisa katika mechi ya saba, lakini wapo wanaoonekana hawako mbali naye kama Sergio Aguero mwenye mabao 6 na Leonardo Ulloa na Berahino wenye matano.
Idadi ni kitu muhimu kabisa kwa kuwa ndiyo kinachofunga mahesabu, lakini nani mwenye uwezo mkubwa wa kutumia silaha zote tatu, lakini yupi ana uwezo wa kufunga ndani na nje ya 18?
Costa amefunga mabao yake yote ndani ya 18, lakini matatu mguu wa kulia, manne kushoto na mawili ameyashindilia kwa kichwa, hali inayoonyesha ni hatari sana.
Aguero amefunga mabao yote sita kwa mguu wa kulia, tofauti yake na Costa ni kuwa, manne amefunga ndani ya 18 na mawili akiwa nje ya eneo hilo.
Ulloa ambaye anatikisa pia ambaye ana mabao matano, mawili kafunga na mguu wa kulia, moja kushoto na mawili kwa kichwa, kama ilivyo kwa Costa, yote amekwamisha akiwa ndani ya 18.
Wafungaji hawa ukiwafuatilia utagundua kuna burudani ya aina yake kwa kuwa kila mmoja ana ujuzi wa aina yake, unaotofautiana na mwenzake na kusababisha ushindani baina yao kuwa mkali na mwisho hujui nani atamaliza akiwa mfalme wa kutikisa nyavu England. Angalia takwimu.

                                  MECHI   DAKIKA  MGUU KULIA  KUSHOTO  KICHWA  NDANI YA 18   NJE MABAO
Diego Costa           7       585             3                4                2                 9               0       9 
Sergio Aguero        8       532            6               0                0                  4               2      6
Leonardo Ulloa      7        568           2                1               2              5                   0       5
Berahino                 7        628           4                0               1               5                  0       5  
Naishmith             7        567             2                1               1               4                  0      4
Pelle                        7        630             2                1                1               4                 0       4


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic