Yanga imeendelea kujifua
jijini Dar es Salaam na nahodha wake amesema wako fiti na hakuna majeruhi hata
mmoja.
Nadir Haroub ‘Cannavaro’
amesema wachezaji wako ngangari na wanaendelea na mazoezi kwenye Uwanja wa Boko
Veterani jijini Dar es Saalaam.
“Tuko vizuri tunashukuru na
mazoezi yanaendelea vizuri pia.
“Lengo ni kufanya vizuri,
hivyo tunajituma,” alisema Cannavaro ambaye anajiunga na Yanga baada ya
kuitumikia Taifa Stars kiufasaha na kuifungia bao wakati ikiitungua Benin kwa
mabao 4-0 katika mechi ya kirafiki, juzi.
Yanga inajiandaa na mechi
dhidi ya watani wake Simba, Oktoba 18.









0 COMMENTS:
Post a Comment