Wachezaji wa Yanga wameendelea na mazoezi kwenye Kiwanja cha Boko
Veterani, huku wakionyesha kujiamini kwa kiasi kikubwa.
Yanga inajiandaa kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya
Simba ambayo itapigwa Oktoba 18 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Tayari watani wao Simba wako jijini Johannesburg kwa ajili ya
kambi.
Chini ya Maximo, Yanga walifanya mazoezi wakionyesha kuwa na
uhakika wa wanayoyafanya.
Kocha Maximo naye alionekana kuzungumza na msaidizi wake, Leonardo
Leiva mambo kadhaa huku wakitikisa vichwa.
Hata wakati wa kuchezea mpira, wachezaji wa Yanga walionekana kuwa
na kasi iliyowafurahisha mashabiki waliojitokeza kwa wingi.
0 COMMENTS:
Post a Comment