YP (KULIA) WAKATI WA UHAI WAKE. HAPA ALIKUWA NA KUNDI LA WANAUME WALIPOTEMBELEA OFISI ZA GLOBAL PUBLISHERS. |
Msanii YP aliyekuwa katika kundi la Wanaume
TMK amefariki dunia.
YP alikuwa akisumbuliwa na kifua kwa muda
mrefu, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Aliyekuwa bosi wake, Said Fella amesema
mipango ya mazishi inafanywa kwa kushirikiana na ndugu zake.
Bado haijajulikana kama mwili wa marehemu
utapelekwa kwao Mbeya au atazikwa jijini Dar.
YP alichipukia akiwa na msanii mwingine Y
Dash ambao waliokuwa chipukizi katika TMK Family kabla ya kusambaratika na
kuunda makundi mawili.
0 COMMENTS:
Post a Comment