Na Saleh Ally
MANCHESTER United wamejibandika jina la
Mashetani Wekundu, wakitaka kuonyesha kuwa wao ni watu hatari, ukikutana nao
uwanjani, ujue umekwisha.
Kwa zaidi ya misimu 15, Manchester United
haijawahi kuwa na hofu ya juu dhidi ya wapinzani wao Manchester City kama
ilivyokuwa msimu uliopita na huu wa 2014-15.
Man United, wana hofu, kila wanapokutana na
jirani zao hao wanajua ni shughuli pevu na msimu uliopita walianza kuipata ‘fleva’
ya woga. Msimu huu imepanda juu zaidi kwa kuwa hawakiamini kikosi chao.
Kesho ni mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England
kwa msimu huu ambayo inawakutanisha wapinzani hao wakubwa wa Jiji la
Manchester, huku Man City wakiwa nyumbani kwao Etihad.
Tayari wameharibu mara mbili mfululizo,
wamefungwa mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya West Ham, wakavuliwa ubingwa wa
Capital One Cup kwa kufungwa na vibonde Newcastle. Sasa wakubali tena kuendelea
kuwaudhi zaidi mashabiki wao kwa kupoteza “Manchester Derby?” Hali ya Man City
inazidi kuongeza ugumu na ubora wa mechi hiyo kesho.
Kwa Man United, ndiyo wapo kwenye drip ya
nafuu, wanaanza kuinuka, lakini ‘derby’ imewakuta mapema. Wana uwezo wa
kuchagua, waitumie kuinuka au ndiyo wazame kabisa.
Msimamo bado unawashitaki kwa kuwa wako katika
nafasi ya nane wakiwa na pointi 13, wameshinda mechi tatu tu katika tisa,
wamepoteza mbili. Wakati Man City wako katika nafasi ya tatu wakiwa na pointi
17, wameshinda 5 na kupoteza mbili tu katika tisa.
Ukipita kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar
es Salaam, mechi hiyo ya kesho tayari ni gumzo. Lakini mashabiki wengi wa Man
United wana hofu, wanaona si kikosi kile cha enzi ya Alex Ferguson.
Kiasi fulani, sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea
katika mechi iliyopita, kidogo inaamsha morali, kwamba huenda wakajaribu.
Ukweli, soka haiko hivyo na mechi ya watani,
haipimwi kirahisi hivyo na mwisho, kikosi cha Man United, kadiri siku
zinavyosonga, kinazidi kuwa kipana na inawezekana kikafanya vizuri kwenye mechi
hiyo.
Nahodha wake, Wayne Rooney atakuwa anarejea
uwanjani kutoka kwenye adhabu ya kadi nyekundu, usisahau katika mara zote 167
timu hizo zilizokutana kwenye michuano yote, Rooney ndiye mfungaji anayeongoza kwa
kufunga mabao mengi, amepachika 11.
Giggs ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi
zaidi, kapiga 36 lakini kesho atakuwa kwenye benchi katika nafasi ya kocha msaidizi.
Rekodi zinaonyesha Man United ndiyo wamekuwa
wakiitawala zaidi mechi hiyo ya watani ingawa jibu la kesho haliwezi kuwa rahisi
kama wengi wanavyotathmini.
Man United ina kikosi chenye wachezaji wengi wazoefu
wa mechi kubwa kama Rooney, Radamel Falcao, Angel Di Maria, Robin van Persie,
hakuna shaka kuwa wana uwezo wa kuwaangusha akina Kun Aguero, Yaya Toure, Vincent
Kompany na wenzake. Yeyote anaweza kupoteza.
TAKWIMU:
MARA YA KWANZA:
Zilikutana Novemba 12, 1881 zikitumia majina
ya West Gorton (Man City) 0–3 Newton Heath (Man United).
ZIMEKUTANA:
Mara 167
USHINDI:
Man United (69), Man City (48) na sare (50).
MECHI NYINGI:
Ryan Giggs (36)
MABAO MENGI:
USHINDI MKUBWA:
United 1–6 City (1926)
United 0–5 City (1955)
United 5–0 City (1994)
United 1–6 City (2011).
0 COMMENTS:
Post a Comment