Kocha Msaidizi wa Yanga, Leonaldo Leiva ameamua kubaki nchini
baada ya mkewe kutua jijini Dar es Salaam.
Wabrazili wengine wanne wa Yanga, Kocha Marcio Maximo, kiungo
Andrey Coutinho na mshambuliaji Geilson Santana ‘Jaja’, wote wako nchini Brazil
kwa ajili ya mapumziko.
Lakini Leiva pekee ameamua kubaki baada ya mkewe kumfuata jijini
Dar.
Taarifa za uhakika kutoka
Yanga zinasema Leiva anatarajia kutembelea mbuga za wanyama pamoja na
kisiwa cha Zanzibar akiwa na mkewe.
“Kweli Leonaldo yuko hapa Dar es Salaam, ameamua kubaki na
mapumziko yake yatakuwa hapa.
“Wengine watatu wameondoka nchini kwa ajili ya haya mapumziko ya
siku chache. Watakaa na familia zao kidogo kwa kuwa kipindi cha Krismasi
watakuwa hapa.
“Hivyo waliona vema wakakutana na familia zao, kabla ya kurudi na
kuendelea na kazi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment