Kocha Patrick Phiri wa
Simba, amekabidhi ripoti yake ya mechi saba za mwanzo za Ligi Kuu Bara.
Ripoti hiyo tayari
imeufikia uongozi wa Simba na imeelezwa leo mchana ulikaa na kuipitia.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kupokelewa kwa bripoti
hiyo.
“Kweli amekabidhisha ripoti
na uongozi unaanza kuifanyia kazi,” alisema Hans Poppe.
Ripoti hiyo inajumuisha
mechi sita za mwanzo ambazo Simba ilitoka sare na moja ya mwisho ambayo
waliibuka na ushindi dhidi ya Ruvu Shooting.
Imeelezwa baada ya uongozi
wa Simba kuipitia, utakutana na kocha huyo na kujadili mambo kadhaa.
Hata hivyo haijaelezwa
itakutana naye lini ingawa kuna taarifa anaweza kuondoka kesho au keshokutwa kwenda kwao Zambia.
0 COMMENTS:
Post a Comment