November 22, 2014


Bosi Mkuu wa kikosi cha vijana cha Simba chini ya miaka 20, Nico Kiondo, amesema kuwa hawezi kumtumia kiungo mpya, James Msuva katika kikosi chake kwenye mechi za maandalizi kuelekea Kombe la Uhai mpaka pale watakapokamilisha usajili wake.


Msuva ni mdogo wa kiungo wa Yanga, Simon Msuva ambaye Simba imeonyesha nia ya kumnasa katika kipindi hiki cha dirisha dogo la usajili lililofunguliwa tangu Novemba 15, mwaka huu.

Licha ya kuendelea kufanya mazoezi na timu hiyo, Msuva hakuweza kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Tabata Academy uliochezwa katikati ya wiki hii kwenye Uwanja wa Kinesi, Shekilango jijini Dar kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria.

Msuva Jr alikuwa jukwaani pamoja na wachezaji wengine ambao hawakuwa kwenye mipango ya kucheza mchezo huo na alipoulizwa alisema kuwa anasumbuliwa na Malaria.

Mara baada ya mechi hiyo, Kiondo alisema kuwa Msuva ni miongoni mwa wachezaji wazuri wanaojitahidi lakini hataweza kumtumia kwenye mashindano ya Uhai kutokana na usajili wake kutokamilika.

“Unajua nina wachezaji wengi wazuri katika kikosi cha vijana ambao wote wanajituma akiwemo Msuva lakini siwezi kumtumia katika michezo ya kirafiki kwa sababu bado viongozi wanaendelea na mazungumzo ya kumsajili, sasa ni vigumu kuendelea kumpa nafasi katika mechi za kirafiki kutokana na kuwa timu inajiandaa na mashindano ambayo yataanza wiki ijayo,” alisema Kiondo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic