Shirikisho la Soka Africa (Caf) limemteua mwamuzi kutoka nchini Tanzania, Samwel Mpenzu
kushiriki kwenye mchujo wa kuwapata waamuzi watakaochezesha michuano ya Kombe
la Mataifa ya Afrika (Afcon 2015) inayotarajiwa kufanyika mwakani nchini
Equatorial Guinea.
Iwapo
Mpenzu atafuzu mchujo huo, atakuwa ni Mtanzania wa tatu kuchezesha michuano
mikubwa kama hiyo barani Afrika, waamuzi wengine waliowahi kuchezesha ni Omar
Abdulkadir na Ferdinand Chacha aliyechezesha Afcon (U-21).
Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Salumu Umande, amesema kuwa wameshapokea taarifa hizo za
kuteuliwa kwa Mpenzu na tayari ameshawasili nchini Misri kwa ajili ya mchujo
huo ambao unatarajiwa kufanyika kati ya leo (Jumamosi) na kesho.
Alisema
kuwa iwapo atafanikiwa kufuzu kwenye mchujo huo, atapata nafasi ya moja kwa
moja ya kuchezesha fainali hizo, kitu ambacho kitakuwa ni hatua kubwa kwa
waamuzi wa Tanzania kwani kwa miaka mingi hakuna mwamuzi hata mmoja kutoka
Tanzania aliyepata nafasi hiyo.
“Ameshawasili
Cairo kwa ajili ya mchujo huo, kama atafanikiwa atapenya moja kwa moja
kuchezesha fainali hizo, tunamuombea apite kwani itakuwa ni hatua kubwa kwenye
nyanja ya waamuzi wetu wa Tanzania,” alisema Umande.
0 COMMENTS:
Post a Comment