November 13, 2014


Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesikitika kusimama kwa Ligi Kuu Bara akisema walikuwa wameanza kupata mwendo.

Phiri amesema walianza kwenda kubadilika baada ya mateso makali ya sare mfululizo.
“Nafikiri tungeedelea kucheza, ingekuwa lahisi zaidi kubadilisha matatizo.

“Hata hivyo si jambo baya, wakati wa mapumziko wachezaji pia wanaweza kuutumia kwa kutafakari,” alisema.

Phiri anatarajia kuondoka nchini wakati wowote kurejea kwao Zambia kwa ajili ya mapumziko.

Simba ilicheza mechi sita mfululizo na kuambulia sare, lakini iliamka katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting kwa kuitundika kwa bao 1-0 na kuandika ushindi wake wa kwanza msimu huu ambao uliamsha faraja kubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic