Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio
Maximo na wachezaji wake wawili, Jaja na Coutinho wametua nchini Brazil salama
salimi.
Taarifa zinaeleza kocha huyo na
wachezaji hao wawili, wameanza mapumziko rasmi ya siku 10.
“Kweli kocha, Jaja, Coutinho
wameanza mapumziko na watarudi nchini baada ya Novemba 20.
“Pia wachezaji wengine wamepewa
mapumziko na wataanza mazoezi pamoja,” kilieleza chanzo.
Maximo, Jaja na Coutinho
hawatakaa Brazil muda mrefu kwa kuwa wanatakiwa kurejea mapema kuanza maandalizi
ya mechi ya kirafiki dhidi ya Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment