Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri ametua nchini kimyakimya na yu tayari kuanza kazi mara moja.
Phiri anatarajia kuanza kazi ya kuinoa tena Simba ambayo inajiandaa katika mechi ya kirafiki ya Bonanza dhidi ya Yanga, Desemba 13.
Phiri aliyeondoka nchini na kwenda nyumbani
kwao Zambia kupumzika, amerejea na kuanza majukumu yake huku kazi kubwa ikiwa
ni kuhakikisha wachezaji anaowataka wanatua Msimbazi.
Simba itacheza na Yanga katika mchezo wa Nani
Mtani Jembe, Desemba 13, mwaka huu, ambapo timu hiyo imepanga kujiimarisha
kabla ya mchezo huo.
Klabu hizo mbili kwa sasa zipo katika harakati
za kufanya usajili mzito wa kuhakikisha zinaimarisha vikosi vyao ili kuleta
ushindani katika ligi.
Rais wa
Simba, Evans Aveva, amefunguka kuwa tayari wameshakabidhiwa na Phiri kila kitu,
hivyo kazi iliyobaki kwa sasa ni yao.
Bosi aliyeingia madarakani hivi karibuni,
alisema kuwa baada ya kocha huyo kutua, walifanya mazungumzo naye na kukubaliana
nini cha kufanya kwa ajili ya kuiboresha timu yao kabla ya mchezo huo wa kirafiki wa bonanza.
Aveva alisema wanahitaji kusajili wachezaji
muhimu katika usajili wa dirisha dogo ili kuwakomesha watani wao Yanga ambao wamekuwa
wakiwaita wazee wa sare.
“Tunahitaji kikosi imara cha kuifunga Yanga, lazima tuwafunge katika mchezo huo,” alisema Aveva.
Wakati huohuo, kikosi hicho kinatarajiwa
kuweka kambi ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya kujiandaa na mchezo
huo.
0 COMMENTS:
Post a Comment