November 29, 2014


Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazili, Marcio Maximo, amemwambia kiungo wake mshambuliaji, Mganda, Hamis Kiiza kuwa atampa nafasi ya mwisho ya kucheza kwenye kikosi chake kwa sharti la kuonyesha ubora wake ndani na kama akizingua basi atamuondoa kabisa.


Mganda huyo, hivi karibuni alitangaza kugomea kuongeza mkataba mwingine kwa kuwa huu wa sasa unaelekea ukingoni akiwa amebakiza miezi sita inayotarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, kwa kile alichodai kocha wake hampi nafasi ya kucheza.

Maximo amesema kuwa kwenye kikosi chake anampanga mchezaji anayejituma na anayetimiza majukumu anayompa.

Maximo alisema, hayupo tayari kuharibu kibarua chake kwa kumchezesha mchezaji kwa kumfurahisha, hivyo atampanga mchezaji mwenye bidii na kujituma kwa kuanzia mazoezini na katika mechi.


“Mimi siku zote ninampanga mchezaji anayejituma, anayetimiza majukumu yake na mwenye bidii, mimi ninapenda kuendelea kuifundisha Yanga, hivyo sitakubali kuharibu kibarua changu kwa kumpanga mchezaji kwa kumfurahisha.”

1 COMMENTS:

  1. Maximo acha utani kwani Jaja alikuwa anajituma?!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic