Ripoti ya ukaguzi wa mahesabu ya kampuni binafsi (jina tunalo), imeonyesha Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) lilitoa kitita cha dola 90 (Sh milioni 153) kumlipa
Kocha Kim Poulsen.
TFF
ililazimika kumlipa Poulsen kutokana na uamuzi wake wa kuvunja mkataba na
ripoti hiyo ya ukaguzi wa fedha imeeleza hivyo.
Poulsen
alikubali kuondoka baada ya kutaka kulipwa kutokana na mkataba wake lakini bado
hakuna uhakika kama kweli alilipwa kiasi hicho kikubwa cha fedha kwa ajili ya
kuvunja mkataba.
Nafasi
ya Mdenishi huyo, imechukuliwa na Mart Nooij raia wa Uholanzi ambaye tokea
aanze kuinoa Stars, pia hakuna mabadiliko makubwa ukilinganisha na yale ya
Poulsen.
Mara
kadhaa, TFF wamekuwa wakisisitiza kutotaka kuizungumzia mikataba kwa madai kuwa
ni siri kati yao na mhusika. Hata hivyo fedha hizo nyingi kwa ajili ya kuvunja
tu mkataba, zinatia hofu.
Ripoti
hiyo ya ukaguzi wa mahesabu ya udhamini kati ya TFF na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), imeonyesha kuna uchakachuaji mkubwa wa fedha.
Baadhi
ya matatizo ni pamoja na kununuliwa kwa magari mawili aina ya Toyota Hiace
ambaye wakaguzi hawakuyaona na moja halina hata jina la TFF na badala yake
linamilikiwa na mtu aitwaye Juma Shariff.
0 COMMENTS:
Post a Comment