Mchezaji bora wa mwezi
Oktoba ambaye ni kiungo wa Klabu ya Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, leo
anatarajiwa kukabidhiwa tuzo yake wakati timu yake itakapokuwa kwenye uwanja
wake wa nyumbani Azam Complex, Chamazi kumenyana na Coastal Union.
Sure Boy alichaguliwa kuwa
mchezaji bora baada ya kupata kura nyingi kutoka kwa wataalamu waliowekwa na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika kila mechi ili kumchagua mchezaji bora
wa mechi kisha mwisho wa mwezi kuchaguliwa mchezaji bora.
Mkurugenzi wa mashindano
wa shirikisho hilo, Boniface Wambura, alisema kuwa mchezaji huyo atakabidhiwa
tuzo hiyo kabla ya mchezo wao utakaowakutanisha na Coastal Union.
“Mchezaji huyo atakabidhiwa
zawadi yake kutoka kwa mdhamini wa ligi ambayo ni tuzo pamoja na fedha shilingi
milioni moja, atakabidhiwa kabla ya mechi,” alisema Wambura.
Wakati huohuo, shirikisho hilo
limetangaza rasmi tarehe ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili ambalo
linatarajiwa kufunguliwa ifikapo Novemba 15 hadi Desemba 15, mwaka huu.
“Pia tunazitangazia klabu
kuwa dirisha dogo la usajili litafunguliwa rasmi mwezi huu tarehe 15 na
litaenda mpaka kufikia mwezi ujao, Desemba 15 ni muda wa kila timu kufanya
usajili ili kuimarisha vikosi vyao kwa ajili ya mzunguko wa pili,” alisema
Wambura.
0 COMMENTS:
Post a Comment