Wachezaji wa Simba wameendelea na mazoezi ya gym pamoja na uwanjani jijini Dar es Salaam.
Chini ya Kocha Mkuu, Patrick Phiri na Msaidizi wake, Selemani Matola wamekuwa wakiendelea kufanya mazoezi huku wakiwa gym wakitumia vyuma zaidi.
Lengo ni kuimarisha miili yao iweze kupambana vyema na mikiki ya ligi na baada ya hapo wamekuwa wakianza mazoezi ya uwanjani.
Kesho Simba A itawavaa Simba B katika mechi ya kirafiki itakayochezwa Ununio jijini Dar es Salaam.
0 COMMENTS:
Post a Comment