Shirikisho
la Kimataifa la Kimataifa (Fifa) limesogeza mbele kozi ya ukufunzi ya
utawala wa mpira wa miguu iliyokuwa ifanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es
Salaam.
Kwa
mujibu wa Fifa, kozi hiyo sasa itafanyika Machi mwakani katika tarehe
itakayotangazwa baadaye.
TFF
imepokea maombi ya zaidi ya washiriki 40 kwa ajili ya kozi hiyo
itakayoshirikisha washiriki 30. Kutokana na maombi kuzidi idadi ya nafasi
zilizopo, FIFA itafanya mchujo wa washiriki.
0 COMMENTS:
Post a Comment