December 5, 2014


Mshambuliaji anayetajwa kuondoka Yanga, Said Bahanuzi, amezua hofu baada ya kutoonekana mazoezini kwa siku mbili mfululizo huku benchi la ufundi likiwa halina taarifa zake.


Bahanuzi ambaye hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuwaniwa kwa karibu na Stand United ya Shinyanga, amekuwa na wakati mgumu Jangwani mbele ya makocha watatu waliopita klabuni hapo huku akibaki kuwa staa wa michuano ya Kagame ya mwaka 2012 ambapo aliibuka mfungaji bora.

Straika huyo hajaonekana mazoezini tangu juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Loyola, Mabibo na inaelezwa kuwa benchi la ufundi halina taarifa zozote juu yake.


“Mhh..! kweli Bahanuzi hayupo na hajaonekana mazoezini kwa siku mbili, sijajua yupo wapi,” alisema mtoa habari wetu.

Taarifa nyingine zilieleza alikuwa mgonjwa na aliomba ruhusa, upande mwingine umeeleza yuko katika maandalizi ya kutua Stand United ya Shinyanga na simu yake haikupatikana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic