Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire,
inawezekana ndiye anayeongoza kwa kuwa na simu nyingi kati ya wasemaji wote
hapa Tanzania.
Msemaji huyo mwenye mbwembwe nyingi, anamiliki
simu tano za mitandao yote ambayo inapatikana hapa nchini na anasema hata ukiingia
mtandao mwingine atanunua simu nyingine.
Masau amesema anamiliki simu hizo kwa kuwa hataki sana usumbufu na analahisisha watu kumpata.
“Ninamiliki simu tano kama unavyoona. Unajua
kila mtandao nina simu yake, Tigo, Zantel, Airtel, Vodacom na Smart, ndiyo
maana unaona ninamiliki simu nyingi.
“Hapa nawapa hata waandishi urahisi
wanaponitafuta kwa ajili ya stori,” alisema.
Alipoulizwa kwa nini asitumie simu zenye laini
mbili na kuendelea alijibu: “Hapana, napenda sana simu zenye laini moja,
naamini hizi ndiyo imara hata kama utaongezeka mtandao mwingine kesho nitanunua
simu nyingine.”








0 COMMENTS:
Post a Comment