Kipa wa Azam FC, George Munishi ametua kwenye
mazoezi ya Yanga kwa ajili ya kufanya majaribio ya kuichezea timu hiyo
inayojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na mechi ya Nani Mtani Jembe.
Munishi ni mdogo wake na kipa namba moja wa
Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, tayari amefanya mazoezi kwa siku mbili juzi
Jumatano na jana Alhamisi chini ya kocha wa makipa, Juma Pondamali.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka ndani ya
benchi la ufundi la timu hiyo, kipa huyo anaangaliwa uwezo wake ndani ya uwanja
na kama akiwashawishi viongozi basi watamsajili, ikiwa ni siku chache tangu
kuwepo na taarifa kuwa klabu hiyo inaweza kutoendelea kuwa na kipa Juma Kaseja
ambaye haonekani mazoezini.
“Benchi la ufundi limetoa nafasi kwa makipa kwa
ajili ya kuwasajili katika dirisha dogo na yule atakayeushawishi uongozi
atapewa mkataba wa kuichezea Yanga.
“Tayari kipa George ambaye ni mdogo wake Dida,
ametua kwenye mazoezi ya Yanga kwa siku mbili mfululizo kwa ajili ya kufanyiwa
majaribio,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa Dida kuhusiana na hilo, alisema: “Ni
kweli kabisa mdogo wangu George ameanza mazoezi na Yanga na tayari amefanya kwa
siku mbili, kabla ya kufanya majaribio Yanga alikuwa akiichezea Azam FC ya U14.
“Ana umri wa miaka 16, anasoma Shule ya Sekondari
ya Chamazi, aliondoka Azam FC baada ya kubanwa na masomo yake,” alisema Dida.
.jpg)







0 COMMENTS:
Post a Comment