December 8, 2014


Kiungo wa Simba, Haruni Chanongo amegoma kujiunga na kikosi cha pili cha timu hiyo.


Chanongo alipata sekeseke la kusimamishwa hivi karibuni baada ya kushutumiwa anacheza chini ya kiwango lakini baadaye likatoka tamko kuwa anahitaji kurejea kucheza kikosi B cha timu hiyo kwa ajili ya kuimarisha kiwango, kitu ambacho Chanongo hakukifanya.

Aidha, tangu kutolewa kwa agizo hilo, nyota huyo hajaonekana kwenye mazoezi ambayo yanaendelea kwenye Uwanja wa Mwenge Shooting, Dar huku kocha mkuu wa kikosi hicho, Nicholas Kiondo akisema kuwa hajamuona na wala hajui yuko wapi.
Kutokana na hilo tayari uongozi wa Simba unafanya mpango wa kukaa chini na mchezaji huyo kwa mara nyingine na kuangalia tatizo ni nini mpaka anashindwa kutii kile anachoelekezwa kufanya.
Kiondo amesema Chanongo hajaonekana katika mazoezi ya kikosi chake na kusema kuwa hawezi kulitolea ufafanuzi zaidi suala hilo kwani hana taarifa zake rasmi.
“Mhh…! Nimekuwa nikisikia taarifa zake kuwa anatakiwa kuwa na sisi, lakini sijamuona na wala hajawahi kufika mazoezini kwangu. Siwezi kulizungumzia zaidi maana sijapewa taarifa rasmi kuhusu yeye,” alisema Kiondo.

Alipoulizwa Msemaji wa Simba, Humphrey Nyasio, alisema: “Chanongo anatakiwa kuwa na kikosi cha vijana na tayari tulishampa taarifa kuhusu kwenda huko lakini kweli mpaka sasa hajajumuika na kikosi kama alivyoelekezwa na anaonekana kama hataki, kwa hiyo uongozi sasa utazungumza naye juu ya hilo na kujua kwa nini amekataa kutii agizo hilo.


“Lakini pia kwa kukataa agizo hilo, Chanongo anakuwa kama anajichelewesha mwenyewe kurejea kurudi kikosi cha wakubwa kwa kuwa alishaambiwa atafanya kule kwa siku chache kisha mwalimu Phiri (Patrick) atamrejesha mara moja.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic