Kitasa mpya wa Mbeya City, Juma Nyosso, amefunguka kuwa amefurahi kujiunga na timu
hiyo lakini kubwa alilonalo kwa sasa ni kupambana kurejesha heshima ya timu
hiyo iliyopotea hivi karibuni.
Beki
huyo wa zamani wa Simba na Coastal Union, amejiunga na timu hiyo hivi karibuni
kwa mkataba wa mwaka mmoja akiwa mchezaji huru baada ya kukaa nje ya michuano
ya Ligi Kuu Bara kwa takribani miezi mitano.
Nyosso
alisema kuwa kikubwa kwake kwa sasa pamoja na wachezaji wenzake ni kuhakikisha
wanairejesha timu hiyo katika hadhi yake ya awali kwa ajili ya kupata mafanikio
stahiki ya kitimu, kisha ya kwake binafsi yatafuata.
Mbeya
iliyokuwa moto wa kuotea mbali msimu uliopita na kumaliza nafasi ya tatu katika
msimamo wa ligi, safari hii imekuwa na matokeo ya kusuasua na kuishia kuburuza
mkia baada ya mechi saba za awali za ligi.
“Nimefurahi
kurejea kwenye ligi lakini kikubwa kwa sasa ni kuhakikisha naisaidia vilivyo
timu yangu ili irejeshe heshima yake, naamini tutashirikiana vema na wachezaji
wenzangu katika hili, timu ikishakaa pazuri, heshima ya mchezaji mmojammoja
itakuja baadaye,” alisema Nyosso, beki wa zamani wa timu ya taifa, Taifa
Stars.







0 COMMENTS:
Post a Comment