Kiungo mpya mkabaji mpya wa Yanga, Mbrazili,
Emerson De Oliviera, amewaangalia viungo wenzake, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite
na Said Juma na kutamka kuwa ana kibarua kigumu cha kupata namba kwenye kikosi
cha kwanza cha kocha Marcio Maximo.
Emerson alitoa kauli hiyo wikiendi iliyopita
mara baada ya mechi ya kirafiki kati ya Yanga na Express ya Uganda kumalizika
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar. Yanga ilishinda bao 1-0.
Emerson
amesema atapata kibarua kigumu kutokana na uwezo mkubwa wa viungo hao
aliowakuta kwenye kikosi hicho baada ya kuwaona mazoezini na kwenye mechi dhidi
ya Express.
Alisema amepanga kuongeza bidii ya mazoezi
kuhakikisha anamshawishi kocha wake aingie kwenye kikosi cha kwanza, baada ya
kuishuhudia mechi dhidi ya Express akiwa jukwaani.
“Yanga
nimekuta ushindani mkubwa wa viungo, ni timu yenye wachezaji wenye kasi na
viwango vikubwa ambao ninaamini watanipa ushindani wa namba.
“Lakini hiyo hainipi hofu ya mimi kuingia kwenye
kikosi cha kwanza, ninaamini nina uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo,
kikubwa nilichopungukiwa ni pumzi na stamina, vitu ambavyo nilivifanyia kazi katika
mazoezi ya wiki iliyopita.
“Mchezaji kama Niyonzima, Twite na Said
niliowaona mazoezini na kwenye mechi, wote wana viwango vya kustahili kuanza
kwenye kikosi cha kwanza, hivyo nina kazi kubwa ya kumshawishi kocha anipange,”
alisema Emerson.







0 COMMENTS:
Post a Comment