December 27, 2014

STAND UNITED.
Pambano la Ligi Kuu Bara kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Stand United, limeahirishwa.


Pambano hilo limeaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Turiani na kusababisha Uwanja wa Manungu kujaa maji.
 
MTIBWA SUGAR.
Awali pambano hilo lilisimama kwa dakika 15, lakini kamisaa Bile Mwilima alipoona alama za uwanja zimefutika, pamoja na utelezi kuwa wa hali ya juu, akatangaza kuliahirisha.

Kutokana na hali hiyo, pambano hilo ambalo hadi linavunjika lilikuwa sare ya bila mabao, litachezwa kesho saa mbili asubuhi.


Kwa mujibu wa kamisaa huyo pambano hilo litachezwa kesho kuanzia dakika ya 6.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic