![]() |
| HANS POPPE. |
Uongozi wa klabu ya Simba, utaendelea
kumlipa mshahara mshambuliaji wake, Paul ‘Modo’ Kiongera licha ya kumuondoa
kikosini.
Kiongera ameondolewa kwenye kikosi cha Simba
na nafasi yake imechukuliwa na Mganda, Danny Sserunkuma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe aiambia SALEHJEMBE kuwa mkataba wao na Kiongera utaendelea kuwa hai.
| KIONGERA. |
Hans Poppe amesema wataendelea kumlipa
mshahara Mkenya huyo kama kawaida wakati akiendelea na matibabu.
“Bado yuko chini yetu, sisi ndiye
tunaogharimia matibabu yake, pia tutaendelea kumlipa mshahara hadi hapo
atakaporudi maana tunamhitaji, tatizo limekuwa ni majeraha tu.
“Mapumziko yake ni marefu baada ya kutibiwa,
zaidi ya miezi mitatu. Hatuwezi kuendelea kuifunga nafasi wakati tunaihitaji,
hivyo tumekubaliana vizuri na yeye ameleelewa,” alisema Hans Poppe.
Kiongera aliumia katika mechi ya kwanza ya
Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.








0 COMMENTS:
Post a Comment