Na Saleh Ally
Saa chache tu baada ya kutua nchini India, mshambuliaji wa Simba, Paul Kiongera amefanyiwa upasuaji wa goti.
Upasuaji huo imefanyika nchini India katika Hospitali ya Manipal iliyo katika jiji la Bangalore.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Musleh Al Rawah alifunga safari hadi kwenye hospitali hiyo na kumjulia hali.
Al Rawah alisema: “Kwa kweli kila kitu kimekwenda vizuri na tayari ameishafanyiwa upasuaji.
“Tulifika pale hospitali na kufanikiwa kumjulia hali, imani ni kuwa atapona haraka.”
Kiongera ambaye alisajiliwa na Simba akitokea KCB ya Kenya alishindwa kuichezea kutokana na kuumia katika mechi ya kwanza ya ligi.
Katika mechi hiyo dhidi ya Coastal Union, Kiongera ndiyo alikuwa ameingia lakini akagongana na kipa Shabani Kado na kuumia.








0 COMMENTS:
Post a Comment