![]() |
| TWIGA STARS. |
Michuano ya Taifa ya mpira wa miguu kwa
wanawake ya Proin Women Taifa Cup inaanza rasmi Desemba 28 mwaka huu kwa mechi
ya ufunguzi kati ya timu za mikoa ya Mara na Mwanza itakayochezwa Uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Kombaini za mpira wa miguu za
mikoa yote ya Tanzania Bara zitashiriki mashindano hayo yatakayochezwa kwa
raundi mbili mwanzoni, na baadaye hatua ya robo fainali hadi fainali.
Mashindano hayo
yanayodhaminiwa na kampuni ya Proin Promotions Limited, kuanzia hatua ya robo
fainali, mechi zote zitafanyika jijini Dar es Salaam.
Meneja Biashara wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania, Peter Simon Shankunkuli aliishukuru kampuni ya
Proin ambao ni watengenezaji, wazalishaji na wasambazaji wa filamu za
kitanzania kwa kuwezesha mashindano hayo kufanyika kwa mara ya kwanza.
Proin Promotions imekua
ikivumbua vipaji mbalimbali vya uigizaji na sasa imeamua kujikita katika mpira
wa miguu ili kuweza kuvumbua vipaji kwa wachezaji wa kike.
Shankunkuli alisema nafasi
bado zipo kwa wadhamini watakaoguswa na mashindano hayo, kwa kuwasiliana na TFF
au Proin Promotions Limited kwa maelezo zaidi.








0 COMMENTS:
Post a Comment