Kocha mkongwe nchini,
Abdallah Kibadeni ameonya wale wanaotoa taarifa bila ya kuwa na uhakika.
Kibadeni amesema
amesitikishwa sana na usumbufu walioupata watu jana kwa yeye kuzushiwa kifo.
“Kweli imenisikitisha sana,
ndiyo maana nimeamua kusema tena. Si jambo jema na vizuri mtu ukiambiwa kitu
uulize kupata uhakika.
“Kutangaza kifo cha mtu si
jambo dogo, pia si sahihi kama hauna uhakika.
“Hivyo nawaasa watu
kuhakikisha jambo kabla ya kulitangaza au kuandika. Nimeambiwa kuna mtandao
ndiyo ulianzisha hilo jambo, basi vizuri watu wafuate weledi,” alisisitiza
Kibadeni.
Jana zilizagaa taarifa
kwamba Kibadeni amefariki dunia jambo ambalo si kweli.








0 COMMENTS:
Post a Comment